21 November 2013

MAJERUHI ALIYEPIGWA RISASI AFARIKI DUNIA, TAZAMA NA PICHA YA MPENZI ALIYEPIGA RISASI NA KISHA KUJIUA MWENYEWE..!!


MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam jana amefariki dunia leo asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu waliofariki katika tukio hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar es Salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na Kablu ya wazee huku maziko 




yakisubiri kutengemaa kwa afya ya mama mzazi.familia imekiri kuwa Christina na 


Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana 


kutokana na vurugu alizowahi mfanyia siku za nyuma. 



IKUMBUKWE Tukio la shambulizi la 
risasi lililotokea hii Novemba 19, 2013  asubuhi Ilala Amana jirani na 


Hoteli ya MM na Klabu maarufu ya wazee

limesababisha vifo vya watu wawili na kuacha majeruhi watatu wawili kati
yao
wakiwa taabani.



Taarifa za awali za Polisi zinapasha kuwa, Watu
walio poteza maisha katika tukio hilo ambalo lilikuwa ni la mtu aliyetambulika


kwa jila la Godfrey Munisi kuwapiga risasi wana familia lilisababisha kifo cha

Alfa Alfred na liliwajeruhi Francis Khiranga Shumira , Christina Alfred, Hellen Elieza Newa.




Taarifa hizo zinasema kuwa Mfyatua risasi huyo
ambaye baade alijiua nayeye, Godfrey Munisi alikuwa na uhusiano wa karibu na


Christina Alfred Newa. 




Katika tukio hilo, ambalo linaelezwa kuto tofautiana
sana na lile la Mwanahabari ufoo Saro lililotokea miezi ya hivi karibuni,


muuaji alimjeruhi Nshumila kifuani  na

mama yake Christina  alijeruhiwa maeneo
ya begani na hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.




Huku Christina akijeruhiwa mkononi na mguuni
ambapo alitibiwa katika Hospitali ya Amana na Kuruhusiwa kurudi nyumbani huku mdogo


wa Christina, Alfa Alfred akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali.




Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa
wa benki ya Barclays  ya jijini Dar es Salaam. Shumira ni baharia 


kitaaluma na inaelezwa kuwa ni raia wa Kenya.
CREDIT : MROKIM

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname