![]() |
| Diamond na bwana harusi Peter Okoye ambaye inadaiwa alishangazwa na uwepo wa Diamond katika harusi yake. Mmm! Majanga! |
Baada
ya maneno kuwa mengi kuhusu kivazi alicho vaa Diamond aka Prezident WCB
kwenye harusi ya Peter Okoye wa kikundi cha P Square mwandada
mtangazaji, Salma Msangi ameamua kuandika yake kuhusu issue nzima ya
Diamond kuwa harusini hapo na kivazi chake hicho kilicho zua gumzo.
Nanukuu kutoka kwa Salma Msangi:
"Nilitaka
mmalize nyie kwanza kuongea sasa ni zam yangu, Nilihoji Mie katika
Post ya Diamond Kuonekana kwenye harusi ya Peter wa P’Square, Je Kaka
kaalikwa au kavamia maana kivazi kilienda kinyume na waalikwa. sasa leo
imedhihirika ukweli kuwa bwana huyu alivamia baada ya bwana harusi
mwenyewe kumkana live kupitia Radio mara baada ya kuwasili nchini kwa
ajili Ya show yao kubwa iliyofanyika Leader Club Jumamosi na kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
Katika
Mahojiano hayo yaliofanyika East Africa Radio Mtangazaji alimuuliza
Peter Ambaye ndio alikuwa bwana harusi wiki moja iliyopita wakati
anafanya ndoa ya kimila kama Kuna Mwanamuziki kutoka Tanzania
Alimualika? Bahati mbaya kwa Diamond Peter alishangazwa na uwepo wake na
kuonyesha kutomfahamu msanii huyo hata baada ya kuchezewa wimbo wake.
kwa lugha ingine tunaweza sema Diamond Alivamia Harusi Hiyo Na ndio
maana hata kivazi chake kilileta utata kutokana na kutokuwa na Card
ambayo ingemuonyesha Angalau Dress Code
Haikuwa
Kitu Kibaya Diamond kuhudhuria Harusi Hiyo ila kwasababu kwetu ni
msanii mkubwa lazima tuhoji na tujue maendeleo yake na kafikaje lakini
pia kutokana na harusi yenyewe aliohudhuria kuwa ya wasanii wa kubwa
Afrika kila mmoja alikuwa na shauku ya Kufahamu Lolote. So kwasababu
Diamond ndio alipost Picha Hizo basi angesema mapema ilikuwaje kuwaje
akawepo leo aibu hii isingemkuta
Mbwembwe zikizidi mara ingine zinaweza kukushusha
Diamond Washabiki wako wanakupenda sana sana usiwaangushe basi." Mwisho wa kunukuu.
Dah majanga haya jamani eeee why???
source-jestina-george

No comments:
Post a Comment