Mume wa mtu, Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema baada ya kunaswa gesti
mume wa
mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu
aitwaye Rehema ambao wamenaswa laivu wakifanya ‘mambo’ gesti.
Wawili
hao walinaswa hivi karibuni kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue
Roze maeneo ya Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.
Habari
zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya
leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu
hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo. NA GPL
Ilielezwa
kuwa baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono
ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa
imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP
Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini,
vijana wa OFM walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha
uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika
nje nje!
Wakati
huohuo, kijana mwingine wa OFM aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya
baa hiyo ili kupeleleza bei zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei
kwa kuwa alikuwa na changudoa kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na
wengine waliokuwa wanatoka nje ya eneo hilo.
TAARIFA POLISI
Baada ya
kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa
Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye
aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua
askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.
Ilipotimia
usiku wa manane, ndipo zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu
kuingia ndani ya baa hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya
gesti.
Akiwa
ndani, paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye
chumbani huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha
zoezi kufanyika tu.
KAZI IKAANZA
Kufumba
na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba
na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja
wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Katika
pekuapekua hiyo ndipo mume huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa
mtu huku wote wakiomba msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo
haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika
kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie
hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na
familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
“Chondechonde
mimi nina ndoa na familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu.
Naombeni tuyamalize kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa
polisi, utetezi ambao haukumsaidia.
Katika
mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa
upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
“Hatujazitumia
sisi hizi, tumezikuta humuhumu chumbani. Lakini nawaombeni sana,
msinipeleke polisi nina ndoa yangu. Naombeni mnisamehe kwa sababu mume
wangu atanirarua. Ninyi wenyewe mnajua ndoa ilivyo ngumu, tafadhali
naomba mnisitiri,” alisikika mwanamke huyo.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na
kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana
kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua
kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.
Mbali na
hao, oparesheni hiyo pia ilimtia nguvuni meneja wa eneo hilo, Emmanuel
Mpinge, ambao wote kwa pamoja walifikishwa kituoni na kufunguliwa kesi
yenye namba BUG/RB/13114/2013 - KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA 19/10/2013.
No comments:
Post a Comment