IDADI ya wajawazito nchini wanaojifungua
mapacha walioungana au wenye ulemavu inazidi kupanda ambapo mwishoni
mwa wiki iliyopita, Pili Hija (24), mkazi wa Jang’ombe, Zanzibar
alijifungua watoto walioungana, kinachosikitisha zaidi mmoja alikuwa ni
kiwiliwili.
Pili alijifungua mapacha hao saa 1:00
asubuhi ya Agosti 18, 2013, nyumbani kwake na baadaye kupelekwa kwenye
Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar baada ya watoto kuonekana si wa
kawaida.
Kufuatia matukio kama hayo, Ijumaa
Wikienda lilichimba kwa undani ili kubaini nini husababisha wanawake
kubeba ujauzito wenye matokeo ya mapacha walioungana au mtoto mmoja
kulemaa kiungo chochote cha mwili.
Mtaalam mmoja aliyesomea mambo ya afya
ya uzazi ambaye aliomba hifadhi ya jina, ndiye aliyefunua siri hii nzito
ambayo wanawake wengi nchini hawaijui isipokuwa kwa kusoma habari hii
leo.
Mtaalam huyo alivitaja vidonge maarufu
kwa matibabu ya tumbo la kuendesha viitwavyo Flagyl au Metronidazole
kuwa ndivyo vinavyosababisha matatizo hayo.
Alisema vidonge hivyo ni hatari mno kwa
afya ya mama mjamzito, hasa kwa mtoto aliye tumboni ambaye anatarajwa
kukua na kutoka akiwa amekamilika.
“Wanawake wajawazito, hasa wakiwa wa miezi mitatu ya mwazo, hawatakiwi kabisa kutumia vidonge hivi aina ya Flagyl.
“Hivi vidonge ndivyo husababisha tatizo hili la watoto mapacha kuzaliwa wameungana, kitaalam tunaita Siamese Twins.
“Unajua kwa kawaida mimba huanza kuwa
binadamu kamili miezi mitatu tu ya mwanzo, kitaalam tunaita First
Trimester ambapo kila kitu kinachopaswa kuwa kiungo cha mwilini
hufanyika.
“Baada ya hapo mpaka mwezi wa tisa ni kukua kwa viungo hivyo.
“Katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya
mwanzo kuelekea miezi mingine hadi tisa, mwanamke akitumia Flagyl kwa
sababu viungo vinakuwa, ni rahisi kwa watoto kuungana au kuzaliwa wakiwa
na ulemavu wowote,” alisema mtaalam huyo.
Mtaalam huyo alisema vidonge hivyo
ambavyo hupatikana kirahisi kwenye maduka ya madawa (famasi) hutumiwa
zaidi kwa matatizo ya tumbo, hasa la kuendesha.
“Kwa nchi za wenzetu (zilizoendelea),
ili mtu auziwe vidonge ambavyo vinaweza kuleta madhara lazima awe na
karatasi ya maelekezo ya matumizi kutoka kwa daktari.
“Hakuna daktari wa kweli hata mmoja atakayekubali kumpa Flagyl mwanamke mjamzito, kwa sababu anajua madhara yake,” alisema.
Kuhusu Pili Hija, mapacha wake
walifanyiwa upasuaji Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Kitengo cha Tiba ya Mifupa (Moi) chini ya daktari wa upasuaji wa
watoto, Dk. Zaituni Bokhary.
Mtoto aliyebaki ni yule aliyezaliwa
akiwa na kichwa, ilibidi kumuondoa asiye na kichwa kwa sababu asingeweza
kuwa binadamu kamili.
Dokta Bokhary alisema hii ni mara ya
kwanza kwa jambo hilo kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Mara ya
mwisho lilitokea mwaka 1984.
Source:GPL

No comments:
Post a Comment