Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, leo wamekutana na wanahabari katika msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar, kujadili juu ya kutolewa hospitali katibu mkuu wa jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda. Sheikh Ponda alichukuliwa na polisi kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) jana majira ya saa nne na nusu asubuhi. Katika taarifa yao waliyoitoa kwa wanahabari, viongozi hao wamelaani kitendo hicho alichofanyiwa Sheikh Ponda na kuitisha mkutano wa dharura utakaofanyika Jumapili ya Agosti 18 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Viwanja vya Nuruh Yakin Temeke jijini Dar es Salaam ili kutafakari kwa pamoja na kuchukua hatua.
(PICHA NA DENIS MTIMA / GPL)
No comments:
Post a Comment