Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja/Global Publishers
KUNA
madai kwamba ule ‘mkoko’ wa kifahari wa staa wa maigizo Bongo,
Jacqueline Wolper aina ya BMW X6 lenye namba za usajili T574 BXF
linatarajiwa kuingizwa sokoni wakati wowote na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) baada ya muda aliopewa nyota huyo kulipia deni lake la
kukwepa ushuru wa shilingi milioni 70 kupita bila mwenyewe kusema
chochote.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya
Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni,
umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya
mnada.
Chanzo
kingine kilisema kuwa mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe,
kumekuwa na usumbufu mwingi kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo
baadhi ya matajiri nao wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la
kulinunua.
“Tunashangaa
sana, watu na fedha zao wanakuja hapa kulitaka gari la Wolper, mbona
kuna magari mengi yapo toka mwaka juzi (2009) hawaji kuyanunua au kwa
sababu hili ni la supastaa wa Bongo?” alihoji mfanyakazi mmoja wa TRA
akiomba jina lake lisitajwe gazetini.
Akaongeza:
“Unajua tatizo liko wapi? Baadhi ya wafanyakazi wa TRA nao wamekaa mkao
wa kusubiri siku ya kutajwa kwa tarehe ya kulipiga mnada gari hilo ili
wasuke mipango ya kupata cha juu kutoka kwa matajiri watakawaopigia debe
na kushinda,” kilisema chanzo.
Amani
lilipoongea na Wolper kuhusu gari lake hilo likitaka kujua nini
kitatokea kama hatalikomboa kwa siku alizopewa na TRA ambazo zimepita,
alijibu hivi:
“Kisheria
gari linatakiwa likombolewe ndani ya miezi mitatu lakini mimi
niliandikisha kuwa kwa mwezi mmoja nitakuwa tayari nimemaliza kila kitu.
Hata hivyo, kimsingi na mimi nilimfikisha polisi Ndama Mtoto wa Ng’ombe
ambaye alisimamia ununuzi wake mwanzo hadi mwisho. Kwa hiyo kama ni
kukwepa ushuru ni yeye.
Gari
la Wolper lilikamatwa Juni 28, 2012 kwa madai ya kukwepa ushuru, hadi
Agosti 28, mwaka huu litakuwa limefikisha miezi mitatu ambayo ni ya
kisheria lakini mwezi mmoja aliotaka Wolper uliisha Julai 28, 2012 hivyo
kutoa fursa kwa TRA kutangaza siku ya kulipiga bei.
Wolper alilinunua gari hilo kwa shilingi milioni 250 za Kitanzania likiwa na sifa nyingi tofauti na magari mengine.
No comments:
Post a Comment