MISS
aliyetwaa nafasi ya 2, 2012 katika shindano maalum la mwaka huu,
Hamisa Hassan, anadaiwa kuichafua Miss Tanzania kufuatia kwenda
kushiriki kinyemela Shindano la Miss University Africa 2012 nchini
Nigeria hivi karibuni.
Ilidaiwa
kuwa ili mrembo ashiriki shindano hilo, linalopokea walimbwende kutoka
barani Afrika, lazima atoke kwenye moja ya vyuo vya nchini mwake sifa
ambayo Hamisa hakuwa nayo.
Ilibidi
waandishi wetu wamsake Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim
Lundenga ‘Anko’ ili atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo hasa ikizingatiwa
kuwa, katika shindano maalum la hivi karibuni, Lissa Jensen aliibuka
kidedea na Hamisa kushika nafasi ya pili.
“Ni
kweli Hamisa ni miss wangu, lakini utaratibu wa kwenda Nigeria
kushiriki shindano hilo sifahamu aliutoa wapi? Najua hakuna chuo
chochote anachosoma kwa sasa na wala hakuna mashindano kama hayo
kwangu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wake, Hamisa alipobanwa ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo alikiri kutosoma chuo chochote nchini.
Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua.
Aidha, alikiri kushiriki shindano hilo huku akisema kuwa hayupo tayari kuwataja waliomchagua.
“Ni kweli sisomi chuo chochote ingawa nina mpango huo, ni kweli
nilikuwa Nigeria kushiriki Miss University Africa 2012 na niliingia top
ten, lakini taji lilichukuliwa na mshiriki kutoka Lesotho, lakini
siwezi kuwataja walionichagua kwenda,” alisema.
SWALI: JE, KAMA LUNDENGA AMEKANA, NI NANI ANAHUSIKA??? KWA NINI WALIFANYA SIRI?....
from-mpekuzi
No comments:
Post a Comment