Msuva katika mechi ya leo
Kiiza katika mechi ya leo.
Kikosi Cha Yanga.
MABINGWA
wa soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga SC ya Dar es
Salaam, wameanza vyema ziara yao ya mechi za kujipima nguvu nchini
Rwanda
, baada ya jioni hii kuichapa Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
, baada ya jioni hii kuichapa Rayon Sport mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali.
Yanga
ambao jana walitembelea Ikulu ya Rwanda, walipoalikwa na rais Paul
Kagame kupeleka Kombe la Afrika Mashariki na Kati, ambalo tangu mwaka
2002 mfadhili wake mkuu na mlezi wake ni Rais Kagame, mabao yake
yalitiwa kimiani na Hamisi Kiiza dakika ya pili na Simon Msuva dakika
12.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb ameiambia BIN
ZUBEIRY kwa simu kutoka Kigali kwamba, timu yao ilicheza vema na
kuwazidi kabisa uwezo wenyeji wao na ilikuwa na uwezo wa kufunga mabao
zaidi.
Bin
Kleb alisema kwamba Yanga itashuka tena dimbani kumenyana na Polisi
Jumapili na kwa mujibu wa ratiba ya awali, wanatakiwa kurejea Dar es
Salaam Jumatatu.
Awali,
Yanga ilikuwa icheze pia na mabingwa wengine wa zamani wa Kombe la
Kagame, APR, lakini kutokana na timu hiyo kukabiliwa na mgogoro hivi
sasa uliosababisha kufukuzwa kwa kocha Mholanzi, Ernest Brandy na nafasi
yake kupewa kocha mzalendo kwa muda, imeshindwa kucheza.
Katika
ziara hiyo, Yanga haijaambatana na mfungaji bora wa Kombe la Kagame,
Said Bahanuzi ambaye amebaki Dar es Salaam kwa matatizo ya kifamilia.
Yanga imekwenda Rwanda na msafara wa watu 42, wakiwemo wachezaji 28,
Maofisa watano wa benchi la Ufundi na viongozi wanane.
Viongozi
walio na timu Kigali ni Mwenyekiti, Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti,
Clement Sanga na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini Mama Fatma Karume, Francis
Kifukwe na Seif Ahmed ‘Magari’ sambamba na Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji, Abdallah Bin-Kleb na Salum Rupia.
Yanga
ilitwaa Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo wiki mbili
zilizopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuifunga Azam FC mabao
2-0, ambayo yalitiwa kimiani na Hamisi Kiiza ‘Diego Milito’ na Said
Bahanuzi ‘Spider Man’.
Hiyo
kwa ujumla ilikuwa mara ya tano mfululizo, Yanga inatwaa Kombe hilo,
baada ya awali kuchukua mwaka jana, wakiifunga Simba katika fainali bao
1-0, Uwanja wa Taifa mfungaji Kenneth Asamoah ambaye ametemwa, ingawa
siku hiyo Kiiza pia alifunga bao safi, ambalo refa alilikataa.
Yanga
ilichukua kwa mara ya kwanza Kombe hilo, mwaka 1975 ikiifunga tena
Simba katika fainali, mabao 2-0 wafungaji Sunday Manara ‘Computer’ na
Gibson Sembuli (sasa marehemu) Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Ikachukua tena
mwaka 1993, Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda kwa kuifunga SC Villa
mabao 2-1, yaliyotiwa kimiani na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ (sasa
marehemu) na Edibily Jonas Lunyamila.
Ilichukua
tena mwaka 1999, ikiifunga tena SC Villa, Uwanja wa Nakivubo, kwa
penalti 5-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Yanga
ikisawazisha bao kupitia kwa Lunyamila, baada ya Hassan Mubiru
kutangulia kuifungia Villa, siku hiyo Manyika Peter akicheza penalti
mbili za Waganda.
Aidha,
kwa kutwaa Kombe hilo chini ya Mbelgiji huyo, Yanga imeendeleza rekodi
yake ya kutwaa mataji ya michuano hiyo, chini ya makocha wa kigeni baada
ya mwaka 1975 kuchukua chini ya Tambwe Leya aliyekuwa raia wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kuchukua uraia wa Tanzania,
(sasa marehemu), 1993 chini ya Nzoyisaba Tauzany aliyekuwa raia wa
Burundi kabla ya kuchukua uraia wa Tanzania, mwaka 1999 chini ya Raoul
Shungu wa DRC na mwaka jana chini ya Mganda, Sam Timbe.
Chanzo: Saleh Ally
No comments:
Post a Comment