MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake wameendelea
kuwang’ang’ania wadhamini wa Chama cha Wananchi (Cuf), wakiiomba
Mahakama Kuu iwatie hatiani na kuwafunga kutokana na kitendo cha
kufukuzwa kwao uanachama.
Licha ya wadhamini hao, wengine ni
wajumbe wa Baraza Taifa la
Uongozi la chama hicho akiwamo Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif
Sharrif Hamad. Januari 10, mwaka huu Rashid na wenzake 10 waliwasilisha
mahakamani hapo maombi wakitaka iwaite wadhamani wa chama chama hicho,
wajieleze sababu za kutotiwa hatiani na kufungwa kwa kosa la kupuuza
amri ya mahakama.
Maombi hayo yalitokana na uamuzi wa Baraza la
Taifa la Uongozi la chama hicho wa Januari 4, mwaka huu kuwafukuza
uanachama wa chama hicho na kuwasimamisha wengine. Pia, katika maombi
hayo wanaomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza hilo wa kuwavua
uanachama kwa madai kwamba walikiuka Katiba ya Cuf.
Wakati wa
usikilizwaji wa maombi hayo, Hamad na wenzake katika hoja zao za
maandishi walizoziwasilisha mahakamani kupitia kwa Wakili wao, Augustine
Kusalika wanadai baraza hilo liliwafukuza uanachama wakati tayati
likiwa na amri ya mahakama kuzuia kuwafukuza.
Amri hiyo ya
mahakama ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari mwaka huu kufuatia
maombi waliyoyawasilisha Januari 3, chini ya hati ya dharura. Mwisho
source-mwananchi
No comments:
Post a Comment