20 February 2012

TETESI ZA..MSANII WA BONGO FLAVOUR AMINI KUFUKUZWA THT


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Amini, amesema kuwa ametimuliwa rasmi Tanzania House of Talents ‘THT’, lakini anahisi kama ameonewa kutokana na mabavu yaliyotumika.

Vyanzo vya habari vililipoti kuwa msanii huyo anajandiliwa na uongozi, lakini sasa taarifa iliyopatikana kutoka kwa muhusika

zinadai tayari ameshawekwa pembeni.

Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, huku akitokwa na machozi alisema kuwa uongozi haujatenda haki kwani kosa la kinidhamu alilofanya walipaswa kukaa naye na kuzungumza lakini wameamua kumfukuza kitu ambacho anahisi ameonewa.

“Mimi sioni kama kuwa wema ndani ya THT, ila nachoweza kusema kwamba naenda kufanya muziki wangu na mungu atanijalia tu kwa sababu kila kitu ni mipango,”
Amini  alipigilia msumali wa mwisho.
  

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname