09 January 2012
Beyoncé Beyonce Gives Birth To Baby Girl In Lenox Hill hospital NY
Beyonce na mumewe JAY Z, inaaminika walilipa kiasi cha dola milioni 1.3 za kimarekani, zaidi ya bilioni mbili za kitanzania ili tu kuimiliki gorofa ya nne ya jengo hilo la hospitali ya Lenox hill New York, wawe wao wenyewe, mtu mwingine asiruhusiwe kabisa kuingia. Pia Madaktari na manesi hawakuruhusiwa kufika kwenye wodi gorofa ya nne ambayo Beyonce ndio alikua amelazwa, na madaktari hao walilazimishwa kutoingia na simu zao ndani ya eneo la hospitali ili kuhakikisha hakuna picha inayopigwa. Pia kamera za usalama, za hospitali hiyo zilifunikwa ili tu kuepuka mtoto huyo kupigwa picha, na kwa nje walionekana walinzi wengi wakizunguka eneo la hospitali hiyo. Saa chache tu baada ya kuzaliwa, jina la mtoto huyo wa J & B, lilishika nafasi ya kwanza kwa kuongelewa sana kwenye mtandao wa kijamii wa twitter, huku maneno mengi yakisemwa kwamba jina lake limetokana na imani ya dini ya kishetani, wanayotuhumiwa kuwepo Jay z na beyonce. BLUE: Mwanzoni ilikua amplified kwamba jina lake ni Ivy Blue Carter, lakini baadae ikagundulika kwamba ni Blue Ivy Carter jina ambalo limetokana na majina ya album za JAY Z, THE BLUE PRINT ambazo zinaherufi nne, herufi ambazo zinafanana na tarehe zao za kuzaliwa wote wawili, B (sept) Jay Z (december). IVY: Beyonce aliwah kuliambia jarida la Billboard kwamba kila mtu ana special namba kwenye maisha yake, ambapo kwake na mumewe yao ni 4, hata siku yao ya harusi ni April 4, birthday ya mama yake pia ni January 4, 1954. Ambapo Sasa herufi mbili za mwanzo za IVY zina maana ya namba 4, (IV) kwa kirumi. Pia IVY ni mmea ambao ni mgumu na unaishi muda mrefu, kwa mujibu wa wawagiriki na warumi walioishi enzi hizo, na inaaminika mmea huo, una uwezo wa kuzaa sana, Hivyo imetangazwa kwamba Blue Ivy Carter ni jina sahihi kwa mtoto wa kwanza wa familia ya wafalme wa hip pop. chanzo miladi Ayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment