Jana, Emmanuel
Adebayor aliwakumbusha mashabiki wake kuwa linapokuja suala la kucheza,
kuna mshindi mmoja pekee – yeye. Tottenham iliibuka na ushindi wa mabao 3
kwa 2 dhidi ya Southampton ambapo mawili aliyapachika wavuni mwenyewe.
Kwa baadhi ya watu
uchezaji ule umefananishwa na mtindo ulioanzishwa na Diamond Platnumz,
Ngololo Dance kwenye video yake ya My Number One.
“Adebayor just did that dance u do “number one” after scoring,” aliandika mfuatiliaji wa mechi hiyo ya jana.
Diamond naye aliamua kumshukuru Adebayor waliyekutana naye hivi karibuni nchini Nigeria kwenye harusi ya Peter Okoyo wa P-Square ambako alimuonesha jinsi ya kucheza Ngololo Dance.
Diamond naye aliamua kumshukuru Adebayor waliyekutana naye hivi karibuni nchini Nigeria kwenye harusi ya Peter Okoyo wa P-Square ambako alimuonesha jinsi ya kucheza Ngololo Dance.
‘Das ma Brother @sea25 …. Appreciate so much king…. SALUTE,’ aliandika Diamond kumshukuru Adebayor.
Hata hivyo wengi
wamepinga mchezaji huyo kutumia uchezaji wa Ngololo na kwamba mara zote
hucheza hivyo.’Ile style anacheza tangu yupo arsenal bwan co ngololo cc
mashabik wa arsenl tunmjua yule,’ ameandika shabiki mmoja.
Katika hatua nyingine
Adebayor ameishutumu Tottenham kwa kumkosea heshima. Mchezaji huyo
mwenye miaka 29 hakujumuishwa kwenye picha rasmi ya pamoja ya club hiyo
na alikuwa akifanya mazoezi mwenyewe kipindi Andre Villas-Boas alikuwa
meneja.
“Ilikuwa ngumu,”
alisema Adebayor. “Nilipokuwa naenda mazoezini na kuona picha ya timu
ambayo mimi sikuhusishwa, hiyo ilionesha kukosewa heshima kwa kiasi
kikubwa.”
Adebayor alikaa msimu
mzima kwa mkopo akiwa na Tottenham akitokea Manchester City mwaka
2011-12 kabla ya kujiunga na Spurs kwa mkataba wa £5m August 2012.
Credit-Bongo5
Credit-Bongo5
No comments:
Post a Comment