Kilichonishangaza ni kwamba anadai yeye ni modo lakini picha alizoweka zimepitiliza hata kwenye huo umodo yaani kajianika mtupuu!
Kwa maelezo yake yeye ni mtanzania sasa bado nashangaa tamaduni zetu hatuna utaratibu
wa kujianika kimauzo namna hii jamani hii si biashara inatafutwa kinguvu maana na namba za simu kaweka!!
Kingine anadai ni mama wa mtoto mmoja..kama ni kweli ni mama ina maana hafikirii mtoto wake siku za usoni akikumbana na picha za mama yake mtupu hivi atajisikiaje na kujifunza nini? Hivi tunatengeneza kizazi cha aina gani? Jamani kina dada tubadilike tunajirahisha sana
No comments:
Post a Comment