24 October 2013

TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI




Tatizo la uchafu ukeni
Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano,
ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na
wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au kahawia,

yanatoa harufu kali na yanawasha, basi


hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao
UTOKO.


Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemuza siri ni njia inayowezesha viungo vyamuzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki yadamu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa.
Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi.
Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye
rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.
Sababu za kutokwa na uchafu huo Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za
siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans  Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.
Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususani
mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bacteria wanaosababisha harufu mbaya.
 
 Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na
ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu) kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki
au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu. Wakati mwingine uchafu
wenye rangi kama ya kijani hutoka
-Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri,
mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda
sehemu za siri.
- Mwanamke anapoona
anatokwa na ute uliochanganyikana na damu
hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine
ya Vaginosis.
- Maumivu makali wakati wa
tendo pia ni dalili za ugonjwa
huu.

Matibabu
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya
vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na
daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha
juu ya magonjwa ya wanawake. Dawa za
kupaka  na dawa za
kumeza huweza kumaliza tatizo hili.


Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila
kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa
daktari au nesi.


Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi
ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza
vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke
kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za
kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye
maji machafu ili kusafisha wenyewe
huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za
kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi
asali na vingine vingi naomba niseme kuwa
njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini
madhara yake ni makubwa kama hivyo
kuanza kutoa harufu mbaya.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname