01 February 2016

RAY C AWASHUKIA GLOBAL PUBLISHER KWA KUTOA HABARI DHIDI YAKE JUU YA KURUDI KUBWIA UNGA

Yule mdada kiuno bila mfupa! Rehema Chalamila a.k.a Ray c Ameahidi kupambana na Global publishers mahakani kwa madai ya kuzushiwa habari katika ukurasa wake wa insta ameandi haya

"Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadamu mwenzangu anadiriki kuni niharibia jina langu ili yeye apate kula! Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu? Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu bila hata ya aibu bila hata ya picha ya kuisapoti habari hiyo yaani ni ujinga ujinga tuu umeunganishwa na picha yangu yaani bila hata woga mmechukua picha yangu kwenye insta page yangu tayari mmeshapata story ilimradi mniharibie tu maisha yangu nyie mpate pesa mimi nife maskini! Kama kweli mnauhakika na mlicho kiandika kwanini hamkuweka picha yangu ni kivuta hayo maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni cha daladala,mmepiga picha ya kituo cha daladala cha mkunguni bado mkaona haitoshi mkaaingia kwenye page yangu insta mkachukua picha nilio jipiga mimi mwenyewe na kuitungia story kulichafua jina langu tena ndio kwanza nahangaika kurudi kwenye kazi yangu haki amungu sijawahi kusikia nyie global mmeandika story kuhusu faundation yangu na mambo mazuri nilio fanya japo mnajua kabisa nimewaokoa vijana zaidi ya sabin kutoka kwenye madawa ya kulevya na wanatumia methadone na wako fit je mnajua hilo? Sijawahi ona mmenichangia hata nauli ya kwenda kila siku kwny dose japo kila siku inatakiwa niende na ukikosa ni mateso makali huu ni mwaka wa tatu natumia dawa tuu its not easy ni mateso makalo lakini am fucking hard working kuhakikisha sikosi kwenda kuchukua dawa! Mimi ni mwanamke jasiri naparangana na haya madawa kuhakikisha nayapinga vikali na kamwe sitarudi nyuma hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu! WEWE SHIGONGO UNAMKOSEA SANA MUNGU UNAJIFANYA MLOKOLE Lakini kazi yako ni kuharibia maisha ya wengine unasahau kuwa malipo ni hapa hapa duniani,mimi ni kapuku tu sina mbele wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia kaburi angali ni mzima na wewe Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua kazi yako nimesoma habari yako nimejua ni mvivu wa kufuatilia habari chimbo langu la unga lajulikana sasa kwanini hukunipiga picha nikiwa navuta unga unaenda kupiga picha kituo cha daladala bwege wewweee! NITAPAMBBA NA NYIE MAHAKAMANI" Ray C

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname