02 February 2016

MWILI WA KIJANA MAARUFU SANA HAPA MJINI DAR MAREHEMU CALVIN KAVISHE KUAGWA DAR KESHO LIVE!!MWILI wa aliyekuwa Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa fani ya Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Calvin Kavishe
unatarajiwa kutolewa heshima za mwisho Kesho mchana.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi baba wa marehemu,Nicolasi Kavishe alisema ibada ya kuaga mwili wa marehemu Calvin itafanyika kuanzia saa Sita mchana Katika Kanisa la Mtakatifu Thomas More lilipo eneo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar Es Salaam.
Kavishe alisema baada ya Misa kumalizika watu watapata fursa ya kutoa heshima za mwili kwa mwili wa marehemu na Kisha mwili huo kusafirishwa siku hiyo hiyo kuelekea Rombo Mkuu - Shindi Kati Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya Mazishi yanatarajiwa kufanyika Alhamisi 4/2/2016 saa nane mchana.
Calvin Ambaye alikuwa akitarajia kuhitimu shahada yake ya sheria Julai maiti yake imeifadhiwa Katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alifariki usiku wa kuamkia Januari 31 Mwaka huu, kwa ajali ya Gari Katika eneo la Salenda Bridge.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0714 774494

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname