21 January 2016

Wadau wakutana kujadili njia mahususi za kuboresha mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye majiji

 
Wadau wa mazingira kutoka idara na wizara mbalimbali za
serikali na mashirika binafsi wamekutana Januari 20, 2016 kujadili njia
mahususi za kuboresha mazingira na kukabilaiana na athari za mabadiliko ya
tabianchi kwenye majiji
 Majadiliano hayo ni hatua moja wapo ya uanzishwaji wa mfuko
wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na lengo la kukusanya
pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi
katika Manispaa ya Ilala
 Mradi huo unafanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya ilala na ForumCC
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava akifungua
mkutano huo wa wadau ambao umewashirikisha pia watendaji wa serikali na
mashirika yasiyo ya serikali kutoka katika wizara na idara mbalimbali,  kwa lengo la kujadili kwa pamoja namna ya
kushirikiana na kupata njia ya pamoja ya kuboresha mazingira na kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo mafuriko, magonjwa na uharibifu wa
miundombinu.
Wadau wakifuatilia Mkutano huo
 Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava (katikati)
akiwa na viongozi wa Forumcc wakati wa mkutano huo, kuanzia kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi katika Ofisi ya Makamu wa
Rais, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais,
Julius Ningu wakati kuanzia kulia ni Afisa Miradi Forumcc, Fazal Issa na Mwenyekiti
wa bodi ya forumcc, Yusta Kibona
 Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dr.
Julius Ningu akifafanua jambo wakati wamkutano huo
Meneja Miradi Forumcc, Rebecca Muna akielezea jambo wakati wa mkutano huo
 Picha ya pamoja
 Profesa Robert Kiunsi kutoka Chuo cha Ardhi akiwasilishwa
mada kuhusu atharai za mabadiliko ya tabianchi na namna ya kubabiliana na
athari hizo
 Amy Faust Kutoka Benk ya Dunia akiwasilisha mada ya mifano
ya miradi ya kuboresha mazingira katika majiji ilivyofanikiwa katika nchi
nyingine huko Ulaya, mifano ambayo inaweza kutumiwa pia hapa nchini
 Francis Gowele, Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala akitoa
report ya mazingira katika manispaa hiyo
 Mwezeshaji wa mkutano huo Abdallah Henku akielezea jambo
wakati wa mkutano huo. Picha zote na Tabianchi blog

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname