31 January 2016

Top 10 ya nyumba za kifahari zaidi zinazomilikiwa na mastaa wa soka

Wachezaji mpira wa miguu ni watu ambao wamekuwa wakimiliki fedha nyingi kutokana na kulipwa mishahara mikubwa kwa wiki, ni kitu cha kawaida kwa mchezaji mpira kulipwa pound 100,000/= kwa wiki ina maana kwa mwezi analipwa pound 400,000/= ni zaidi ya bilioni moja ya kitanzania.
Hivyo wengi wao huwa wanaishi maisha ya juu kulingana na mishahara yao wanayolipwa, kwa mujibu wa mtandao wa therichest.com mwishoni mwa mwaka 2014 walitoa list ya nyumba kumi za gharama zinazomilikiwa na mastaa wa soka wanaocheza soka katika nchi tofauti tofauti.
10. Nahodha na mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi ameingia katika hii list na nyumba yake imepewa namba 10 licha ya thamani yake halisi kutokuwa hadharani, lakini inatajwa kuwa moja kati ya nyumba 10 za thamani, ipo katika mji wa Barcelona mji ambao klabu yake ndio ilipo FC Barcelona.
messi-house-2
Nyumba ya Lionel Messi iliyopo Barcelona Hispania
9. Ricardo Kaka huyu ni staa kutoka Brazil lakini pia amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or mwaka 2007 akiwa katika klabu ya AC Milan ya Italia wakati huo lakini kwa sasa anaichezea klabu ya Orlando CityKaka anaingia katika hii List nyumba yake ina thamani ya dola milioni 3.
Kaka-house
Nyumba anayomiliki Ricardo Kaka
8. Andres Iniesta huyu ni moja kati ya wachezaji bora duniani wenye uwezo wa kucheza kwa ufasahaa nafasi ya kiungo lakini bado ni moja kati ya viungo wa kutegemewa katika klabu ya FC Barcelona, Iniesta ni moja kati ya wachezaji wanaomiliki nyumba za kifahari. Nyumba yake ina thamani ya dola milioni 4.6.
Andres-Iniesta-house
Nyumba ya Andres Iniesta wa FC Barcelona
7. Mario Balotelli huyu ni muitaliano mwenye asili ya kutoka Ghana kwa baba na mama, amekuwa maarufu kutokana na uwezo wake uwanjani pamoja vituko vyake ila hayupo nyuma katika masuala ya kumiliki nyumba za thamani, nyumba yake ina thamani ya dola milioni 4.86.
balotelli_house_aerial_0
Nyumba ya mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli
6. Cristiano Ronaldo huyu ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or anaitumikia klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa sasa lakini ni mtu ambaye anamiliki nyumba nyingi za thamani ila hii ni moja kati ya nyumba anazomiliki na inathamani ya dola milioni 6.
ronaldo-house
Nyumba inayomilikiwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid
5. Frank Lampard amewahi kutamba katika klabu ya Chelsea ya Uingereza na timu yake ya taifa ya Uingereza kabla ya hivi karibuni kuamua kwenda kumalizia soka lake katika klabu ya New York City ya MarekaniLampard ana nyumba yenye thamani ya dola milioni 7.
lampard
Nyumba ya Frank Lampard wa New York City
4. John Terry ni nahodha wa klabu ya Chelsea lakini ni moja kati ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza anamiliki jumba lenye thamani ya pound milioni 7.5.
terry-home
Nyumba ya nahodha wa Chelsea John Terry
3. Didier Drogba ndio mchezaji pekee kutoka Afrika aliyeingia katika top ten hii huyu ni staa aliyecheza katika klabu ya Chelsea kwa mafanikio kwani hadi leo yupo katika kumbukumbu ya wachezaji wenye heshima katika klabu ya ChelseaDrogba ana nyumba yenye thamani ya dola milioni 9.
drogba-house (1)
Nyumba ya Didier Drogba
2. Wayne Rooney ni nahodha wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, ni mtu anayeongoza safu ya ushambuliaji kwa klabu ya Man United, anamiliki jumba lenye thamani ya dola 17.83.
rooney-house
Nyumba ya nahodha wa Man United Wayne Rooney
1.David Beckham hadi anastafu kucheza soka alikuwa anatajwa kuwa mchezaji tajiri duniani, Beckham amejipatia umaarufu akiwa katika klabu mbalimbali ikiwemoManchester United kutokana na umahiri wake wa kufunga magoli kwa kupiga faulo.Beckham anamiliki jumba lenye thamani ya dola milioni 20.
beckham-house
Nyumba ya David Beckham

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname