29 January 2016

JARIDA LA BUSINESS TRAVEL LAITUNUKU ETIHAD TUZO YA SHIRIKA LA NDEGE LA MWAKA

Etihad Business Studio

Food & Beverage Manager


Shirika la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la Mwaka wakati wa tuzo za Business Travel 2016. Hafla hii ilifanyika jana usiku katika hoteli ya Grosvenor House iliyopo Jijini London. Tuzo hizi zinatambua makampuni na watu binafsi waliopata mafanikio katika sekta ya biashara ya usafiri na hivyo kuwafanya wastahili kuwania tuzo hizo.

Tuzo hizi zinazoandaliwa na jarida la Uingereza la Buying Business Travel, huwa na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura kubaini washindi. Hii ni mara ya kwanza kwa Etihad kushinda tuzo hiyo, hii ikija siku chache tu baada ya shirika la ndege la Etihad kupokea “Tuzo ya Uvumbuzi katika Usafiri” kutoka tuzo za jarida la Globe Travel katika hafla nyingine iliyofanyika wiki iliyopita London.

James Harrison, Meneja Mkuu wa shirika la Etihad Uingereza, alisema: “Tuzo hii ni ishara ya kutambulika kwa mchango wa Etihad katika sekta ya usafiri wa anga nchini Uingereza. Tunajisikia fahari kubwa sana kutambuliwa katika jukwaa kubwa hivi.”

“Uingereza ni soko muhimu kwa shirika hili na mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kwetu kwani tunasherekea miaka kumi tangu tuanze kutoa huduma zetu kati ya jiji la Manchester na Abu Dhabi. Tunategemea kuzindua huduma ya tatu ya kila siku kutoka uwanja wa ndege Heathrow, jijini London, kupitia ndege aina ya A380 ambayo pia ina huduma ya vyumba ya “Makazi”. Zaidi tunalenga kutoa huduma iliyorahisishwa na inayowaunganisha wageni wetu.”

Shirika la Etihad liliibuka kidedea kutokana na huduma zao za hali ya juu, zikiwemo bidhaa (na vyumba) zilizoingia hivi karibuni sokoni na kuleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga. Hii ikiwa pamoja na kutumia ndege aina ya Airbus A380 na Boeing 787 Dreamliners, bila kusahau vyumba ambavyo vilishakuwa vikitumika na Airbus A330/A340 na Boeing 777.

Mapinduzi haya yametokana na programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa katika Kituo cha Uvumbuzi kilichopo Abu Dhabi na kuongozwa na timu ya ubunifu ya Etihad. Shirika la Etihad linapenda kutoa huduma yenye viwango sawa na hoteli kubwa na sehemu nyingine za kitalii kubwa duniani. Etihad wameajiri wafanyakazi wenye ufundi na uzoefu mkubwa haswa katika safari ndefu kwa mfano wahudumu wakuu walipo katika “Makazi” ya ndege ya A380 kwenda London, Wapishi Wa daraja la Kwanza, meneja wa vyakula na Vinywaji katika “daraja la biashara” na wahudumu wa kutunza watoto wakati wa safari. Wahudumu hawa wamehitimu chuo cha kulea na kutunza watoto Norland huko Uingereza.

Pia shirika la ndege la Etihad lina sehemu ya mapumziko katika viwanja vya ndege wa London Heathrow, Manchester, Frankfurt, Dublin, Paris, Sydney, Washington, D.C. na New York wakati uwanja wa ndege wa Abu Dhabi una sehemu za mapumziko na mapokezi.

Hivi sasa safari za shirika hili zinafika sita kila siku kwenda Uingereza, zikiwa na huduma za moja kwa moja kufika jijini London kupitia uwanja wa ndege wa Heathrow, jijini Manchester na jijini Edinburgh zilizozinduliwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow Jijini London ulipata nafasi ya kuwa kituo cha kwanza kwa ajili ya kuzindua huduma ya ndege za jamii aina ya Airbus A380, ikiwemo huduma ya “Makazi”- ikiwa na vyumba vya kipekee duniani kuwekwa kwenye ndege ya kibiashara yenye ukubwa wa vyumba vitatu huku ndege hii pia ikiwa na vyumba 6 vya “daraja la kwanza”, 70 vya “daraja la biashara” na 415 vya “daraja la uchumi”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname