26 January 2016

HIVI NDIVYO SAMATTA ALIVYOMPIGA CHENGA BOSI WAKE,SASA HUYOOO ULAYA


HATIMAYE mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Mchezaji huyo alitarajia kurejea jana nchini kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka la Ulaya.
Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki.
Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka lake.
Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, ili kucheza soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda huko na alikuwa tayari kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika Aprili.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname