26 January 2016

ETIHAD YAZINDUA HUDUMA ZA SAFARI ZA NDEGE KUFIKA MJI MKUU WA MOROCCO, RABAT Safari kati ya Abu Dhabi na Morocco kufikia tisa kwa wiki

Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto ambayo yalimwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya Rabat na Abudhabi.


ETIHAD YAZINDUA HUDUMA ZA SAFARI ZA NDEGE KUFIKA MJI MKUU WA MOROCCO, RABAT
Safari kati ya Abu Dhabi na Morocco kufikia tisa kwa wiki 
Shirika la ndege la Etihad lazindua rasmi huduma zake za ndege baina ya Abu Dhabi na Rabat, Morocco, ikiwa ni kituo chao cha pili nchini humo.

Ndege ya uzinduzi iliwasili mchana wa leo uwanja wa ndege Sale-Rabat na kupokelewa na mzinga wa maji kama ilivyo desturi ikifuatiwa na wageni rasmi kuwasili, wakiwemo; Lahcen Haddad (Waziri wa Utalii Morocco), na Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaeri.

Huduma hii itakayopatikana mara mbili kwa wiki kupitia ndege aina ya Airbus A340-500 itakuwa yakipekee baina ya Rabat na Abu Dhabi. Tayari kukiwa na safari baina ya Abu Dhabi na Casablanca, shirika litafikisha jumla ya safari tisa kwa wiki kwenda nchini Morocco

Ndege ya uzinduzi (EY615) kwenda Rabat ilibeba msafara ulioongozwa na Khaled Al Mehairbi, Makamu Rais Mambo ya Serikali na Siasa za Anga. Uwakilishi huu ulijumuisha Kapteni Salah Awadh Alfarajalla, Makamu Rais Usalama na Maaendeleo ya Waendesha Ndege Kitaifa; Hareb Mubarak Al Muhairy, Makamu Rais Mambo ya Mashirika na Kimataifa; Ali Al Shamsi, Makamu Rias Operesheni za Kitovu cha Abu Dhabi; Joost Den Hartog, Kaimu Makamu Rais wa Mauzo Duniani; na Amer Khan, Makamu Rais Mashariki ya Kati na Africa Kaskazini.

James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema shirika limefurahishwa na uzinduzi wa huduma ya Rabat kama kituo cha pili katika safari za Morocco.

“Safari hizi mpya zitakazounganisha miji hii zinadhihirisha dhamira ya Etihad kuendelea kujenga mahusiano endelevu na kanda ya ksakazini mwa Afrika na kuimarisha uhusiano kati ya Morocco na Umoja wa Falme za Kiarabu,” alisema.

“Rabat ni mji wa kihistoria unaovutia wanaosafiri kwa ajili ya burudani na biashara. Kwa kupitia huduma yetu mpya, tunalenga kutumia mtandao wetu uliopo duniani kote kukuza wingi wa wasafiri wataotumia njia hii kuingia Morocco. Vivyo hivyo tunarahisisha safari katika Rabat hadi Abu Dhabi pamoja na miji mingine tunayofika, huku tukiwapa wageni wetu fursa ya kufurahia huduma zetu za viwango vya juu zinazotambulika dunia nzima.”

Pamoja na Casablanca, huduma hii ya Rabat itafikisha jumla wasafiri 4,200 kila wiki kwenda Morocco.

Kama UAE, serikali ya Morocco imewekeza sana katika kuiendeleza sekta ya utalii. Mwaka 2010, serikali ilizindua Vision 2020 ikiwa na mpango wa kuifanya Morocco kuwa kati ya sehemu kuu 20 za utalii duniani na hii itachangia kuongeza idadi ya watalii hadi mara mbili ya idadi ya awali hadi kufikia takribani milioni 20 mpaka kufika mwaka 2020.

Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaheri, alisema: “Sina mashaka kwamba safari hizi kati ya miji hii mikuu ya kiarabu zitaimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi katika masuala ya usafiri wa anga. Hii ni hatua nyingine ya maendeleo katika uhusiano kati ya UAE na Morocco. Safari za moja kwa moja zitachangia sana kuleta maendeleo katika biashara, uwekezaji na utalii. UAE na Morocco zimeunganishwa na historia ndefu ya ushirikiano na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizi mbili na utaendelea hivyo katika miaka ijayo.”

“Nimeridhika sana kwa kampuni za UAE zinavyozidi kutazama kwa umakini nafasi zilizopo kushirikiana, kuwekeza na kufanya biashara mjini Rabat. Ni dhahiri kwamba nyakati zijazo jamii za kibiashara zitapata faida kubwa katika nchi hii na tungependa kushuhudia ushirikiano ukikua na bila shaka shirika la Etihad ni mfano mzuri wa hili.”

Huduma hii itakuwepo Jumatano na Ijumaa kwa kutumia ndege aina ya Airbus A340-500 yenye siti 240, 12 za daraja la kwanza, 28 za daraja la bisahara na 200 za daraja la uchimi.

Huduma ya Abu Dhabi-Casablanca imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanzishwa Juni mnamo mwaka 2006. Huduma ya Abu Dhabi-Rabat inawapa abiria chaguo zaidi na njia mbili zinazounganisha Morocco na UAE na imefungua njia kufika sehemu nyingine katika mtandao wa Etihad’ GCC, Bara la Hindi na Asia Kusini Mashariki pamoja na Australia

Shirika la Etihad pia limesambaa kufika Afrika Kaskazini kwa makubaliano ya ‘codeshare’ na Royal Air Maroc, ikiwapa abiria ndege za safari za moja kwa moja kutoka Casablanca mpaka sehemu zingine Morocco kama Agadir, Marrakech and Tangier.
Shirika la ndege la Etihad pia imeongeza huduma zake Afrika kufika Johannesburg, Khartoum, Cairo, Lagos, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam and Mahé in the Seychelles.

Ratiba ya safari katika ya Abu Dhabi and Rabat, kwanzia Januari 15 2016
 Ndege na.
Kuondoka
Kuwasili
Muda wa kuondoka
Muda wa kuwasili
Aina ya ndege
Siku
  EY 615
Abu Dhabi
Rabat
10.00
15.15
A340-500
Jumatano/Ijumaa
  EY 616
Rabat
Abu Dhabi
20.00
07.25  kesho yake
A340-500
Jumatano/Ijumaa

Angalizo: muda wa kuondoka na kuwasili ni kwa muda wa Abu Dhabi

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na  airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com

soma zaidi hapa www.darwaya.com

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname