MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala
imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha
ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.
Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.
Mbele ya Hakimu Flora
Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai mahakama imemkuta
Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.
Mbasha ambaye ni mume wa
muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha anadaiwa kumbaka
shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo la Tabata ambako
alikuwa akiishi naye.
Kesi hiyo ilianza
kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti huyo aliieleza
Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu mbili tofauti
kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Kwa mujibu wa Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186,
kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama ya siri ili
kulinda haki ya binti huyo.
Kesi hiyo itatajwa tena
mahakamani hapo Julai 23, mwaka huu ambapo Mbasha anatakiwa kufika na
mawakili wake ili kujitetea dhidi ya shtaka hilo
No comments:
Post a Comment