TAARIFA KWA UMMA
1. Siku ya Jumapili tarehe
12 Juli, 2015, kulikuwa na habari nyingi za uongo na zenye madai ya kashfa na
maneno ya uchochezi ambayo yalichapishwa katika vyombo vya habari vyenye sifa
mbaya kwa jamii vya Reginald Mengi vilivyo chini ya makampuni ya IPP ambavyo
vilikuwa na vichwa vya habari vya ajabu kama vilivyotoka katika magazeti ya:
a. Guardian On Sunday ambapo kulikuwa na kichwa cha habari
cha “Wakala wa Manji akamatwa katika
njama za kutoa rushwa ya Sh 700m”;
b. NipasheJumapili ambalo lilichapisha kichwa cha
habari cha “Millioni 700/- za Manji
zanaswa hotelini Dodoma”; na
c. Televisheni ya ITV iliyotangaza katika Taarifa ya Habari ya
Jumamosi, Julai 11, 2015 na Jumapili, Julai 12, 2015 ikirudia habari za
magazeti yaliyotajwa hapo juu.
Habari hizi za ajabu zilizotolewa na
vyombo hivyo vya IPP zilianzisha uvumi huo katika mitandao ya jamii ikiwa ni
pamoja na kusambaza picha pamoja na simulizi za uongo wa kuchekesha..
2. Ukweli halisi ni kwamba
tarehe 10 Julai, 2015, Bw. Amit Kevalramani
aliwasili kwa ndege binafsi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ili kupeleka
fedha za kununua mchele na mahindi mkoani
wa Dodoma katika kampuni la M/s Tanrice Grains & Pulses Limited – kampuni tanzu la M/s Quality Group Limited, ambalo Mwenyekiti
wake ni Bw. Yusuf Manji.
3. Bw. Amit Kevalramani alikuwa
akutane tarehe hiyo ya Julai 10, 2015 na watu wenye kuhusika na manunuzi kutoka
kampuni ya M/s Tanrice Grains & Pulses Limited, ambapo Bw. Amit Kevalramani alikuwa amepanga kurejea
kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ndege ya saa 3:30 siku ya Jumamosi,
Julai 11, 2015.
Mkutano huo ulichelewa, na Bw. Amit Kevalramani alipewa tiketi nyingine ya
ndege kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ambayo ingeondoka saa 10:30 siku ya
Jumamosi, Julai 12, 2015.
4. Kunako kama saa 3:30 asubuhi,
Bw. Amit Kevalramani aliondoka katika
hoteli yake, na wakati akielekea kwenye gari alilokuwa amekodishiwa, alivamiwa
na wezi na katika mapambano yaliyotokea, begi moja lililokuwa na fedha
lilichanika, na hivyo kuwafanya maofisa usalama kufika mara moja katika eneo
hilo.
Baada ya kuona njama zao zimekwama,
wezi hao wakajifanya kuwa wafuasi wa CCM waliokuwa wamepanga katika hoteli hiyo
na kuanza kupiga makelele wakisema “rushwa”, jambo ambalo liliwavuta watu wa
vyombo vya habari kwenda hapo.
5. Katika mkanganyiko huo,
Jeshi la Polisi la Dodoma lilikuwa makini katika kufanya kazi yake ambapo
lilizikusanya fedha zote na Bw. Amit Kevalramani akahakikisha fedha zake zote
zipo na zilikuwa salama. Pia, kutokana na maombi yetu, jeshi la polisi lilihakikisha
Bw. Amit Kevalramani anawekwa mahali penye usalama ambapo asingefikwa na tishio
lolote la kuibiwa fedha hizo. Tulifanya hivyo tukijua kwamba kutokana na
habari potofu zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya IPP vya Reginald
Mengi, Bw. Amit Kevalramani (pamoja na fedha ambayo alikuwa amekabidhiwa) vilikuwa
tayari ni lengo la makundi ya majambazi na makundi ya kisiasa yaliyokuwa
yamekata tamaa.
6. Jioni ya Jumamosi, Julai
11, 2015, Bw. Amit Kevalramani alichukuliwa
na maofisa wa kampuni letu la usalama na
siku ya Jumapili, Julai 12, 2015, akiwa na fedha zote kwa kushirikiana na Jeshi
la Polisi la Dodoma ambalo lilithibitisha kwamba fedha hiyo aliyokuwa nayo Bw. Amit
Kevalramani ilikuwa ni halali, na hivyo Bw. Amit Kevalramani akiwa na fedha hiyo,
akasafiri kwa ndege na kurejea Dar es Salaam salama.
7. Kampuni la M/s Tanrice
Grains & Pulses Limited & Quality Group Limited, linatoa shukurani kwa
Jeshi la Polisi Tanzania kwa utatuzi wa haraka wa suala hilo, na linampongeza
Bw. Amit Kevalramani kwa ushupavu wake
wa kukabili jaribio hilo la wizi.
8. Tunachukua fursa hii
kuwakumbusha Watanzania kwamba Reginald
Mengi na Yusuf Manji wana mgogoro kati yao ambao umechukua miaka ipatayo kumi. Majuzi ulipotolewa mwaliko na Yusuf Manji kwa
Reginald Mengi wafanye mdahalo wa moja kwa moja Julai 3, 2015, ili “kuufichua
ukweli” kuhusu jambo hili, Reginald Mengi alikataa. (Kwa maelezo zaidi ingia www.manjivsmengi.com)
9. Habari zilizochapishwa na
vyombo vya habari vya IPP kuhusu suala
hili ni mfano mwingine wa jinsi Reginald Mengi alivyozama katika imani ya
kusema vitu visivyo sahihi siku zote akitumia vyombo vyake vya habari na kutaka kujaribu
kumwonyesha Bw. Yusuf Maji katika mwanga hasi.
Badala ya kufanya hivyo, jamii nayo ni lazima ivilazimishe vyombo vya
IPP kujibu maswali muhimu ya kawaida kabla ya kuyachapisha, kama vile:
A. Ni kwa nini katika
machapisho na taarifa zote kuhusu suala hili, hakuna hata mtu mmoja kutoka
katika Jeshi la Polisi la Dodoma alihojiwa ili kuthibitisha habari
zilizoandikwa na vyombo vya habari vya Reginald Mengi?
B. Je, kampuni la Quality
Group of Companies lenye wafanyakazi wapatao 5,000 humfanya Mengi kuwa na fikra
za ajabu kwamba kila mfanyakazi wa kampuni hilo ni “wakala” wa Bw. Yusuf Manji,
au kwamba kulitaja jina la Mwenyekiti wa klabu ya Yanga huongeza mapato ya
vyombo vyake vya habari?
C. Kwa nini, katika matukio
ya rushwa ambayo huhusisha pande mbili, yaani mtoaji na mpokeaji, vyombo vya
habari vya IPP vilimtaja “mtoaji” tu na si mpokeaji?
D. Kwa nini wakati CCM
inaendesha shughuli zake, Reginald Mengi alitaka ulimwengu usimame na
kufuatilia mambo yake ya kizamani aliyokuwa ameyabuni katika vyombo vyake vya
habari dhidi ya kampuni ya Quality Group ambayo
inashiriki kwa kiwango kikubwa kuimarisha uchumi wa nchi hii?
E. Kwa nini na kwa namna
gani kiasi kidogo cha fedha cha Sh. Milioni 722.5 (sawa na Dola za Marekani 321,000)
kiweze kubadili taswira za kisiasa nchini, kutokana na madai yanayotoka kwa
mmiliki wa vyombo vya habari ambaye hudai kipato chake cha jumla ni zaidi ya
Sh. Trilioni 1.24 trillion au Dola za Marekani milioni 550?
F. Kwa nini mtu ambaye
amekabidhiwa na kampuni la Quality Group kiasi cha fedha ambacho ni sawa na
Dola za Marekani 321,000 tu, achukuliwe kwamba alikuwa anatenda kosa la jinai kuwa
na fedha hizo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Mengi, wakati gharama ya
kuihudumia klabu ya Yanga kila msimu wa ligi katika misimu mitano iliyopita
kiasi hicho cha fedha ni kidogo mno kikilinganishwa na kile kinachotolewa na Quality
Group?
10.
Kuhusiana na mdahalo wa moja kwa moja wa televisheni
uliokuwa umepangwa kufanyika Julai 3, 2015, kati ya Bw. Yusuf Manji, Mwenyekiti
wa Quality Group Limited na Young Africans Sports Club ambapo Reginald Mengi aliogopa kuhudhuria, Bw. Yusuf Manji bado anatoa mwaliko mwingine kwa
Reginald Mengi kuja na ushahidi kwamba
Bw. Yusuf Manji ni mtoa rushwa, na ayaseme yote hayo katika madahalo huo
ili kuwaacha Watanzania waamua wenyewe kuhususuala hili.
.
Tunaamini kwa dhati kwamba kutokana na mwaliko huu wa
Bw. Yusuf Manji, Bw. Mengi atajitoleza na asitake kujificha kwenye vyombo vyake
vya habari anavyovimiliki bali ajitokeze na kuwapa fursa Watanzania kuamua
kilicho kweli badala ya kueneza vitu visivyo sahihi hata kidogo
No comments:
Post a Comment